Na Dixon Busagaga Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mkuu
wa Wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya
ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi.
HALMASHAURI
ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake
wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka
zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha
za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali
teule ya Machame.
Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha mfukuza kazi.

Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi waliostaafu na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.

Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.
0 comments:
Post a Comment