Mtoto mzuri Bongo, Wema Isaac Sepetu.
Nyota na ing’ae! Mtoto mzuri Bongo, Wema Isaac Sepetu ameliambia
Ijumaa Wikienda kuwa hata kama akizeeka na kuwa kikongwe, bado nyota
yake itaendelea kung’aa siku zote wala haitafifia kwani amezaliwa nayo
labda asiwepo duniani.
Wema ameliambia gazeti hili kuwa anamshukuru Mungu kwa kumjalia nyota
hiyo ambayo inawezekana kuna watu wanatamani izimike wakati wowote,
jambo ambalo haliwezekani leo wala kesho na kwa kuwa alitoka nayo
tumboni kwa mama yake, Miriam Sepetu.
“Hata kama watu wataichafua kiasi gani, nyota yangu itaendelea
kung’aa hadi nitakapokuwa mzee. Nitakuwa ni bibi mwenye mvuto na hata
watoto watapenda kusikiliza hadithi zangu,” alisema Wema

0 comments:
Post a Comment