Tuesday, November 24, 2015

Image copyrightGetty
Image captionYahoo yafungia matangazo ya kibiashara
Baadhi ya watumiaji wa barua pepe wa Yahoo nchini Marekani wameripoti kuwa kampuni hiyo ya Yahoo imekuwa ikiwatumia ujumbe unaowataka wadhoofishe programu inayozuia matangazo ya kibishara ndipo waweze kupata ujumbe wa barua pepe.

Yahoo ilisema ilikuwa inafanya majaribio ya bidhaa mpya nchini Marekani.
Watumiaji wa programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara walisema tayari wamefaulu kukabiliana na kizuizi hicho.
Programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara imekumbwa na utata na kampuni za kiteknologia zimekuwa zikielezea maoni yao kwa njia tofauti.
Image copyrightAP
Image captionProgramu ya kuzuia matangazo ya kibiashara imekumbwa na utata na kampuni za kiteknologia
Mnamo mwezi Septemba, kampuni ya Apple iliboresha mfumo wake wa simu za mkononi ili kuruhusu watumiaji wa programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara kuwa na uwezo wa kuutembelea.
Wakati huo huo Google inasema imeanzisha mpango wa malipo kwenye mtandao wake wa YouTube, ambao unawawezesha watazamaji kutoa matangazo yao ya kibiashara kutoka kwenye video kwa malipo ya kila mwezi.
Wakereketwa wa programu ya kuzuia matangazo ya kibiashara wanasema kudhoofisha matangazo hayo huenda kukarefusha huduma ya betri ya simu aina ya smartphone na kupunguza matumizi ya deta kwenye simu za mkononi.

0 comments:

Post a Comment