Saa tisa kamili kikao cha nne cha Mkutano wa kwanza wa Bunge la 11 kitaanza rasmi na kuhutubiwa Rais wa Tanzania John Magufuli.
Mkutano huu utahudhuriwa na viongozi karibu wote wa juu akiwemo Rais wa Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein. Askari wametanda hivi sasa hapa katika viwanja vya bunge kuimarisha Ulinzi.
Kikosi cha Gwaride kipo hapa na hivi punde maafisa usalama wameingia katika ukumbi wa Bunge kukagua hali ya usalama.
Tutaendelea kujulishana hapa kila kinachoendelea hatua kwa hatua kuanzia sasa hadi mwisho wa hotuba hiyo.
========
Bunge limeshaanza na anaapishwa mbunge mmoja aliebaki, ndugu Nchambi. Viongozi kadhaa wamehudhuria hotuba ya leo akiwemo Rais aliemaliza muda wake, Dr. Jakaya Kikwete, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
Tundu Lissu: Napenda tupate muongozo kuhusu baadhi ya wageni kuwakaribishwa ndani, kwa hali ilivyo leo hatuna Rais wa Zanzibar, hatuna makamu wa kwanza au wa pili halali wa Zanzibar, hatuna spika wala baraza la wawakilishi Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar muda wa serikali ya Zanzibar uliisha tangu Novemba 2.
Naibu spika amemjibu kwa kusema kifungu pia kinasema Rais wa Zanzibar anafikia ukomo mpaka Rais mpya anapoapishwa.
Rais John Magufuli amewasili viwanja vya bunge na kukagua gwaride kisha kuelekea ndani kufungua bunge.
Rais wa Zanzibar, Shein anaingia ndani na wapinzani wamegoma kusimama na kuimba 'Maalim Seif'
Baada ya kuingia Rais Magufuli, zomea zomea iliaendelea na spika wa bunge, ndugu Ndugai aliamuru wabunge wote wanaopiga kelele watoke nje na wahusika wakatoka kwa hiari.
Kwa sasa amekaribishwa Rais Magufuli kuhutubia bunge, na anayaongea aliyodhamiria kuyaongea siku ya leo pia Rais Magufuli amempongeza Zitto Kabwe kwa kuwa ni mbunge wa upinzani ambae hajafanya vurugu na kutoka nje na kusema ndio upinzani anaoutaka.
Magufuli anaendelea kuelezea malalamiko kutoka kwa wananchi ikiwemo TANESCO, maliasili na kusema lazima watendaji wanahusika kwani haiwezekani meno ya tembo yakashikiwe Ulaya wakati ni makubwa pia amaongelea mipaka ya hifadhi na wananchi.
Uhamiaji na ajira, kutoa hovyo vibali vya uraia, kushindwa kusimamia vibali vya ajira za wageni, elimu kukiwa na michango mingi isyo na ulazima. Eneo jingine polisi ikiwemo Raia kubambikiwa kesi ikiwemo zimamoto kuchelewa kufika kwenye tukio tena bila maji.
Mahakama, bado kuna malalamiko mengi ucheleweshaji wa kesi. Madini pia imelalamikiwa.
Magufuli: Nina kila sababu ya kulinda muungano wetu, ni azma yangu kuona wananchi wa Bara na visiwani wanafurahia muungano. Serikali ya awamu ya tano itaendeleza utabuni kwa kuheshimu mihimili ya dola. Mahakama tutaipa uzito kwa kusogeza huduma karibu na wananchi.
Mchakato wa katiba, serekali yangu imepokea kiporo, tunatambua kazi kubwa ya wananchi walioshiriki pia tunatambua kazi nzuri ya tume ya kurekebisha katiba na bunge la katiba.
Rais amemaliza kuhutubia bunge na kulifungua rasmi, baada ya hapo spika anawatambua wageni waliohudhuria ikiwemo marais na mawaziri wastaafu kisha anamkaribisha waziri mkuu ili kusitisha bunge.
Kassim Majaliwa: Najua kazi iliyo mbele yangu ni nzito lakini kwa ushirikiano wenu naamini Mungu atanipa nguvu, naahidi ntafanya kazi kwa bidii na maarifa kwa watanzania, awamu hii ni ya kazi tu. Rais ameonyesha muelekeo mzuri na mimi nitaihubiri kauli mbiu hii, nampongeza sana mheshimiwa Rais.
Nimpongeze mheshimiwa Rais kwa hotuba yake nzuri, bunge lina jukumu moja kubwa ya kutunga sheria. Kuna ukweli kwamba kama mbunge anafanya kazi vizuri ataweza kuwa karibu na wananchi na kufikisha mapendekezo yao serikali.
Wakati Kikwete anafingua bunge 2005 alisema wabunge ndio macho ya wananchi, mtafakari kwa kina imani na heshma mliopewa na wananchi. Nafahamu mbunge ana majukumu mengi lakini kubwa ni majukumu yako kwa waliokupigia kura. Ni lazima kama wabunge turudi majimboni na kufanya kazi za wananchi katika kutatua kero zao.
Makundi ya kisiasa kati yetu sasa yaishe, wabunge pia wana majukumu ya kuisimamia serikali kuhakikisha inatoa mchango wake kikamilifu kutumia nyenzo zake. Lengo ni kuitoa Tanzania katika dimbwi la uchumi ulio nyuma, jukumu hili ni letu sote.
Kila mmoja akifanya kazi kwa kujituma naamini tutasonga mbele, tukitaka kusonga mbele lazima tuweke dhamira ya kweli na pasiwe na yeyote wa kuturudisha nyuma na yeyote anaediriki tuhakikishe tunamrudisha yeye kabla ya kuturudisha sisi.
Waziri mkuu ameahirisha bunge mpaka January 26, 2015.

0 comments:
Post a Comment