Na Charles Francis M.
Leo naomba watanzania wenzangu nichambue kama mchambuzi wa kisiasa na siyo kama mlivyo zoea. Lengo langu ni kuonyesha uhalisia tu na kuibua mjadala wa kitaifa juu ya suala hili.
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini
kupitia chama hicho, ndugu Zitto Zuberi Kabwe inasemekana atawasilisha
hoja binafsi katika vikao vya bunge vinavyo tarajia kuanza tarehe
26/01/2016.
Kwa mujibu wa kanuni za bunge, toleo la mwaka 2007 kanuni ya 54 fasili ya 1 ya kanuni za kudumu za bunge zinatoa uhuru wa mbunge yeyote kutoa hoja binafsi na kama itaungwa mkono na wabunge wengi basi inaweza kuundiwa sheria, au kufanywa kama azimio la bunge na hivyo bunge kama mhimili unao jitegemea sawa na Ibara ya 62 katiba yetu ya mwaka 1977 kusimamia utekelezaji, ikiwa utata utajitokeza juu ya kukubaliana basi kura za siri zitapigwa kutokana na uzito wa jambo husika.
Charles Francis nilifuatilia misimamo ya Zitto, Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 Zitto Kabwe akiwa mbunge wa Kigoma kaskazini (Chadema) aliweka msimamo wake wazi wa kukataa kupokea posho za vikao. Pia kuna muda Januari Makamba aliwahi kukataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati aliwahi kukataa posho.
Charles Francis NAMUONAJE ZITTO KABWE ANAPOKATAA KUPOKEA POSHO ZA VIKAO??
Kuna sababu nyingi sana zinazo mfanya Zitto kukataa posho zikiwemo zifuatazo:
1. Kwanza kabisa hii ni "karata ya kisiasa" kwa Zitto binafsi lakini pia ni silaha dhidi ya wapinzani wake kisiasa. Katika hoja hii, msingi wa Zitto utakuwa ni kwamba, kwanini tuchukue posho wakati tuna mshahara? kwanini tupokee posho wakati tuna mikopo ya magari bila riba tena kwa bei nafuu? kwanini tupokee posho wakati tunapewa matibabu bure?
Sasa kwa sababu hizi atapata kuungwa mkono na wananchi LAKINI SI WABUNGE!
2. Pili, Zitto anataka kuaminisha watu kuwa yeye ni mzalendo na mchumi wa kweli. Anataka kuaminisha watu kuwa yeye ana uzalendo kwa kuwa hachukui posho! Zitto anataka kuaminisha watanzania kuwa uchukuaji wa posho ni usaliti katika kuwatumikia wananchi.
3. Tatu, ni silaha ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020! Kuna tetesi kwamba Zitto Kabwe anataka kugombea Urais mwaka 2020. Hili la Kukataa kwake posho za vikao Charles Francis naliona kama ni silaha yake ya uchaguzi na ataitumia kama agenda ya uzalendo na uadilifu katika kampeni zake za kuingia ikulu.
MIFANO YA MSINGI ITAKAYO MPATIA NGUVU "KISIASA" ZITTO KUHUSU POSHO NI HII:
1. Mwaka 2011 serikali ilipokea msaada wa Tshs bilioni 20 kwa ajili ya Sensa ya mwaka 2012 lakini posho za wabunge za mwaka ni sawa na bilioni 28 nje ya marupurupu na fedha nyingine! Hapo utagundua wabunge peke yao "wanatafuna" bajeti nzima ya sensa ya nchi. Hapa tutaondokana na tatizo sugu la "NCHI KUWA OMBA OMBA ULAYA". Hapa Charles Francis naona kuna hoja ya msingi sana!
2. Fedha hizi pia zinaweza kutumika kwa wanafunzi wa elimu ya juu, elimu ya vyuo vya kati, sekondari na hata shule ya msingi kwa maana ya "capitation grants".
3. Utaratibu wa kulipana posho za vikao ni sawa na kupeana "zawadi" wakati ni wajibu wako kufanya jukumu hilo! Hoja hapa inaweza kuwa, kwanini wabunge wasiache kazi kama posho ni ndogo? kwanini bado wanapambana kurudi bungeni?
4. Posho ni kuendelea kutengeneza mfumo wa viongozi matajiri wanaotaka kuwa matajiri zaidi ya wananchi wanao waongoza. Tukumbuke bunge la Kenya lilipotaka kuongeza mishahara, wakenya waliandamana kila kona ya nchi kupinga lakini kwa Tanzania tunacheka na kuona ni kawaida.
5. Huduma za Afya zinaweza kusadiwa kupitia posho hizi na makato mengine ya safari na vikao vya watumishi wa serikali.
Ikumbukwe wabunge wengi baada ya kuzoea kuongezewa posho sasa kupitia bunge la kumi, walitoa mapendekezo yao kwa tume ya utumishi wa Bunge, ya kumlipa kila mbunge mafao ya Shilingi milioni 238 baada ya kukoma kuwa mbunge!
Tukumbuke pia Tanzania ilikuwa ikiagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani (2011-2013). Kiwanda cha kutengeneza LPG kina gharimu Tshs bilioni 35 tu, Wabunge peke yao kwa mwaka wanatumia bilioni 28 kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine. Fedha hizi tukizitafutia mahali pa maendeleo kama nchi hatutafikia malengo ya kufika uchumi wa kati?
SHERIA ZINASEMAJE KUHUSU MISHAHARA, POSHO NA STAHILI ZA WABUNGE??
Hapa Charles Francis nawakumbusha kuwa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeundwa kwa mujibu wa Ibara ya 62 ya Katiba ambapo mshahara na marupurupu mengine ya wabunge yameelekezwa katika Ibara ya 73 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Kutokana na msingi wa Katiba hii, Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Spika, Naibu Spika, Wabunge na Wajumbe wa Tume hulipwa kwa mujibu wa Sheria ya Hitimisho la Kazi ya Viongozi wa Kisiasa Sura Na. 225 ya mwaka 1999 pamoja na Sheria ya Marekebisho mbalimbali Na. 2 ya mwaka 2005.
JE, ZITTO ATAFANIKIWA??
Hapa jibu ni rahisi sana, Zitto hawezi kufanikiwa kwa sababu kubwa mbili:
1. Ni yeye pekee na Chama chake wanao miliki agenda hiyo ya kufuta posho na mpaka sasa bungeni ni yeye peke yake anatoka ACT (yaani chama chake)!
2. Maslahi binafsi ya wabunge wengi. Hapa hata Zitto angefanya nini hawezi kushinda kwa sababu wabunge wa UKAWA wanaonyesha wazi kuwa hawamuungi mkono Zitto Kabwe kwa aina ya siasa anazo fanya. Pia wabunge wa CCM wengi walipendekeza posho ziongezwe hivyo ni ngumu leo waseme zifutwe kabisa na hawa wako wengi zaidi ya 190!
MWISHO: ZITTO ANAJUA HATAFANIKIWA, KWANINI BADO ANA NIA HII?
Hapa jibu ni moja, "Zitto ni mtaalamu" wa kuchanga karata kisiasa! Hapa anajiandaa kukuza jina lake lakini pia kuteka imani za watanzania huku akiandaa mazingira ya yeye kuwa na ushwishi kwa kundi kubwa la vijana na watu wenye uchumi ngazi ya chini kabisa ambao ni wengi katika uchaguzi mkuu 2020.
"kipimo cha mtu yeyote imara ni maamuzi na uwezo wa kusimamia maamuzi yake".
Charles Francis M.
francischarles92@yahoo.com
0752 20 20 52
0715 20 60 48.

0 comments:
Post a Comment