Chama cha ACT-Wazalendo kimeweka rekodi ya kuwa chama cha kwanza cha siasa katika jumuiya ya Afrika Mashariki kuishawishi Serikali juu ya mustakabali wa amani ya Burundi na jitihada za kuwaokoa raia wa Taifa hilo lenye machafuko ya kisiasa.
Huu hapa ni waraka wa ACT-Wazalendo kwa Serikali ya Tanzania,soma.
CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KINAITAKA TANZANIA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKOMESHA MAUAJI NCHINI BURUNDI
1. Chama cha ACT-Wazalendo kinasikitishwa sana na maujai yanayoendelea
nchini Burundi na hasa Mji Mkuu wa nchi hiyo Bujumbura. Hali hii ya
mauaji imesababishwa kwa kiasi kikubwa na uamuzi wa Rais wa sasa wa nchi
hiyo Ndugu Piere Nkurunzinza kuendelea kugombea na hatimaye kuchaguliwa
kuwa Rais wa nchi hiyo katika mazingira yaliyovunja demokrasia na
utawala bora.
2. Tangu machafuko
nchini Burundi yaanze zaidi ya watu 100 wameshauawa kufikia wiki hii na
wengine kadhaa kujeruhiwa. Aidha, wimbi la wakimbizi kutoka Burundi
linarudi kwa kasi na wengi wao wakikimbilia nchini Tanzania.
3. Bahati mbaya sana Jumuiya ya Kimataifa na hasa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambapo Burundi ni mwanachama, haikuchukua hatua za maana za
kuzuia kuchafuka kwa utawala wa kidemokrasia na utawala wa sheria nchini
Burundi, na wala haichukui hatua stahiki kuzuia mauaji yanayoendelea.
Hii ni kinyume kabisa na Mkataba unaounda Jumuiya ya Afrika Mashariki
ambao unatoa kipaumbele cha juu kulinda uhai na haki za raia katika
Jumuiya hiyo
4. Kutokana na hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi, na kwa kuzingatia nafasi ya kihistoria ya Tanzania katika kutafuta na kufanikisha Mkataba wa Amani nchini Burundi, na kwa kuzingatia nafasi yake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika, tunaitaka serikali ya Tanzania, kwa hali kubwa ya dharura, ichukue hatua zifuatazo:
a. Iitake serikali ya Jamhuri ya Burundi kukomesha mara moja maujai yanayoendelea nchini humo na kuwahakikishia raia wa nchi hiyo usalama
b. Iitake serikali ya Jamhuri ya Burundi kuitisha mkutano wa wadau wote wa siasa na utawala nchini humo ili kujadili mustakabali wa nchi hiyo kisiasa na kijamii, ikiwemo uwezekano wa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayosimamia Katiba ya Burundi kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia
c. Itumie nafasi yake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuitakaJumuiya hiyo kuzuia machafuko nchini Burundi na kuhakikisha kwamba utawala wa demokrasia na utawala wa sheria unazingatiwa nchini humo
5. Chama cha ACT-Wazalendo kinasisitiza kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki itakosa uhali wa kuendelea kuwepo kwake kama itaendelea kuwa Jumuiya ya viongozi wa nchi zinazounda Jumuiya hiyo na kishindwa kusimamia haki za kuishi na haki za kiraia za wananchi wa Afrika Mashariki.
Venance Msebo
Katibu wa Kamati ya Mambo ya Nje
ACT-Wazalendo
Jumatano, 16 Desemba 2015

0 comments:
Post a Comment