Posted by Williammalecela.com on Wednesday, December 23, 2015
 |
| Uongozi wa Bendi ya Mashujaa mjini Dar leo wamefanya mabadiliko makubwa ndani ya bendi hiyo ya kumuondoa Urais wa Bendi hiyo Super Star Chalz Baba na kumfanya Rapa Maafurufu wa bendi hiyo Ferguson kuwa ndiye Rais mpya wa bendi hiyo. Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Bendi hiyo Maxi Luhanga, lakini Rais wa zamani wa bendi hiyo Baba ameeleza kufurahishwa sana na uamuzi huo akidai ulikuwa ni mzigo mzito sana mgongoni mwake anashukuru sana kuushusha na kumuachia mwingine na ataendelea kuwa Mwanamuziki mtiifu wa bendi hiyo kama muimbaji wa kawaida. |
0 comments:
Post a Comment