Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watuhumiwa 40 kwa tuhuma za kula njama za kutoa makontena zaidi ya 2500 kinyume na utaratibu wa sheria na kuisababishia hasara Serikali ya mabilioni ya fedha.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema kati ya watuhumiwa hao 26 ni watuhumiwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Watumishi wa tatu kutoka Mamlaka ya Bandari Kavu na wengine 11 ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhusika na makontena 2489.