Mgogoro
wa wakulima na Wafugaji:Hii leo nimefika Mvomero kijiji cha DIhinda
kata ya Kanga kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya tukio baya la
mauaji,Kujeruhi BInadamu na Wanyama lililotokea Desemba 12/2015. "Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima,Hakuna
ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote
yule,njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama
na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa serikali
wa eneo husika hatua kwa hatua,Nawaomba wananchi waache kujichukulia
sheria mikononi.Tunakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii
kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa
maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria." Nimeagiza kupitia kwa
Mkuu wa wilaya na kamati yake ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Mvomero(kwa
husika maeno yote ya Nchi yetu) kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo
yote yenye migogoro,pili wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa
mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa walio jeruhiwa,nimeagiza wapatiwe matibabu kwanza bila kuchelewa na hatua za kisheria kwa wenye hatia zifuate.
Ngombe 79 Wameuliwa na 72 wamejeruhiwa kwa kukatwa mapanga ona hapa live!!
0 comments:
Post a Comment