Posted by Williammalecela.com on Monday, December 14, 2015
 |
SAED KUBENEA MBARONI KWA AMRI YA MKUU WA WIYALA YA KINONDONI PAUL MAKONDA
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) amekamatwa na polisi eneo la viwanda (EPZA) Mabibo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Tukio hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa
kiwanda cha nguo cha TOOKU ambao walimpigia Mbunge wao aende kutatua
mgogoro huo. Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana, akakutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao
na menejimenti ya Kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9. Ilipofika
saa 10:30 Makonda alikuja na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati
ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi. Alitoa amri
wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko kesho na Waziri
wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na waziri wa Afya
wanawake, jinsia na watoto. Alimzuia Mbunge asihutubie kuaga
wananchi aliokuwa nao tangu mchana, Kubenea alisema ni vema aseme neno, Kubenea akaanza kumdhihaki Makonda aliyeamuru Mkutano ufungwe na akaamrisha Kubenea akamatwe mara moja kwa lugha chafu kwa Mkuu wa Wilaya.
Katika tukio hilo Mwandishi wa habari wa Star Tv aliyekuwa anarekodi
tukio hilo alinyang’anywa camera na Polisi. Mwandishi wa habari habari wa MwanaHALISI Josephat Isango
alijaribu kumsaidia mwenzake ili arejeshewe Camera lakini Polisi wa
kituo cha Magomeni walimtisha, na kumtaka kuondoka haraka huku
wakiondoka na aliyenyang’anywa camera. |

0 comments:
Post a Comment