Thursday, December 17, 2015


Kigogo mmoja mzito wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) amezuiwa kusafiri kwenda nje ya nchi yeyey na familia yake kutokana na zuio lilipo kwa sasa kwa watumishi wote wa umma.
Kigogo huyo alikutwa na songombingo hilo baada ya kufika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA)kwa minajiri ya kwenda nje ya nchi kwenda kula bata na familia yake wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka (Xmass na mwaka mpya). Kigogo alidai kuwa safari hiyo alikuwa kagaramikia yeye
mwenyewe kwa pesa yake , wala siyo ya serikali, ila waksema kuwa kwa sasa kuna pini ya kwenda nje
ya nchi kwa mtumishi wa umma .

Kigogo huyo alihojiwa katika chumba maalumu na maofisa wa uhamiaji kwa muda wa kutosha lakini majibu yake yalionekana kujikanganya na kukosa msingi, hivyo aliamrishwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha hapo uwanjani kabla ya kutumbuliwa jipu kama wale wanne wa TAKUKURU walivyotumbuliwa.

0 comments:

Post a Comment