Thursday, December 17, 2015




MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Mjini,Zitto Kabwe amesema kuwa atahakikisha wakati wa vikao vya  bunge vitakavyoanza mwakani anaibana Serikali juu ya baadhi ya mambo hasa katika ufafanuzi juu ya lililokuwa sakata la Tegeta Escrow.

Zitto kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook amefichua kuwa atahakikisha anapambana ili suala hilo linajibiwa kikamilifu na kwamba pesa zote ambazo Serikali inawadai wamiliki wa mitambo ya IPTL zinarudishwa kwa wananchi

Juzi nimewasilisha maswali 5 Bungeni ili yajibiwe na Serikali. Swali la kwanza linahusu umiliki wa IPTL na tshs 8 bilioni tunazowalipa matapeli hao kila mwezi, kwanini mtambo haujamilikishwa TANESCO na anayejiita mmiliki wa IPTL kukamatwa na kushtakiwa. Vile vile ni kwanini Benki ya Stanbic haijachukuliwa hatua kwa kuamuriwa kurudisha Fedha za akaunti ya ‪#‎TegetaEscrow‬. Mambo 2 ( umiliki wa IPTL na kurudisha kwa fedha tshs 320 bilioni) ndio mambo ya msingi kabisa katika suala zima la #TegetaEscrow. Haya ndio nitakufa nayo.

Juzi nimewasilisha maswali 5 Bungeni ili yajibiwe na Serikali. Swali la kwanza linahusu umiliki wa IPTL na tshs 8...
Posted by Zitto Kabwe on 16 Disemba 2015

1 comment:

  1. Mh.....zitto pamoja na haya yote.....lakini pia ungejaribu kujibu hoja ya mh Lusinde.....alipolieleza bunge kuwa ulipokea pesa (rushwa) kutoka kwa mmiliki wa IPTL

    ReplyDelete