Wednesday, December 23, 2015





Msanii Nassib Abdul maarufu kama”Diamond Platinumz” anatarajiwa kuungana na wasanii wenzake akiwemo Msaga Sumu, kikundi cha wakali Dancer kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha maalum litakalofanyika desemba 25 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mratibu wa onesho hilo Juma Mbizo, amesema Tamasha linalenga kuhakikisha mashabiki na wapenzi wa burudani nchini wanamaliza mwaka 2015 na kuingia 2016 kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa mkali huyo wa kimataifa pamoja wasanii wengine wa nyumbani.

Kwa upande wake Diamond Mwenyewe amesema ataendelea kufanya kama kawaida yake kwa kuhakikisha anatoa kile mashabiki wanachokihitaji katika burudani pindi anapokuwa stejini.

0 comments:

Post a Comment