Kim Kardashian West na Kanye West wamempa mtoto wao wa pili jina Saint West.
Kim amethibitisha jina hilo kwenye tovuti yake, siku tatu baada ya kutangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kiume.
Binti wao, aliyepewa jina North West, alizaliwa Juni 2013.
Kim alitangaza kwamba alikuwa ameshika mimba mara ya pili kwenye kipindi chake cha runingani cha Keeping Up with the Kardashians mwishoni mwa mwezi Mei.
Alifichua
kwamba mtoto wake wa pili angekuwa mvulana kwenye ujumbe aliomuandikia
Kanye West kwenye Twitter siku ya kuwakumbuka kina baba duniani, yaani
Father's Day.
Wawili hao hawajasema ni kwa nini wakachagua jina
Saint West lakini baadhi ya ripoti zinasema ni kwa sababu Kim alisumbuka
sana alipokuwa na mimba yake.

0 comments:
Post a Comment