Swali: Kuna baadhi hukutaja,
tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Wabunge wa chama chako
hawana sifa? Usimamizi wa baraza unatarajia zitafanya kazi zake Dodoma
ukiondoa TAMISEMI?
Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko
niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata.
Usiwe na haraka. Kuhusu Dodoma tutatekeleza yaliyoko kwenye ilani ya
chama cha mapinduzi.
Swali: Umesema hakutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?
Magufuli: Niliyowachagua wote wana CCM na wengi wao ni
wabunge, walinadi ya sera hapa kazi na ndio maana haja ya semina
elekezi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya
bilioni mbili.
Manyerere Jackton: Kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kwa kulinganisha na tulipotoka, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?
Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, kwa vile ni mmiliki wa
gazeti huwa unapiga hesabu huwa unapata kiasi gani. Utanisaidia katika
kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za
gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na
bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina
mawaziri wengi mpaka kufikia hata 70, wizara 44, manaibu na mawaziri.
Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34 tu.
Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi
tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina
elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.
Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu na kama wapo
wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa,
contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua,
Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi
tunayowatarajia kuifanya effectivly. Ngoja tukimaliza uteuzi wote
tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi.
Raymond(Uhai Production): Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharejesha zile hela?
Magufuli: Swali hilo kamuulize kamishna wa kodi TRA.
SWALI: Kuna wizara ina mawaziri wawili, huko kazi ngumu?
Magufuli: Kafanye utafiti hio wizara imeunganisha wizara ngapi, utapata majibu.
Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi?
Magufuli: Umekosea hata kupiga hesabu, Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba na sio kumi? Ukipiga utaelewa ni vigezo gani nilivyotumia.
Asanteni sana na ninawashukuru.

0 comments:
Post a Comment