Msanii anayefanya poa na ngoma yake ya TOBA, malikia wa uswazi maarufu
kama Shaa, amefunguka na kusema vitendo vilivyo kuwa vinafanyika katika
video yake havihusiani na Freemason
Shaa amesema amekuwa akiulizwa na watu mbalimbali kuhusu hilo swala na
amekutana na maoni mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii lakini amezidi
kusisitiza kuwa hausiki na masuala hayo kwani kuwa Freemasson lazima uwe
na pesa za kutosha.
Pia shaa ameelezea kuwa yupo mbioni kufanya kolabo na mfalme wa uswazi
Msaga Sumu kwani anaamini msanii huyo anafanya vizuri, hivyo wakikutana
na kufanya kazi pamoja itakuwa vizuri zaidi.

0 comments:
Post a Comment