Posted by Williammalecela.com on Tuesday, December 29, 2015

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baba, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani?
BABA:
Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na
watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta
mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao.
0 comments:
Post a Comment