Posted by Williammalecela.com on Tuesday, December 22, 2015
Magufuli akabidhiwa haya majina ya wauza 'unga'
Kwa muda
mrefu sasa, kumekuwa na mijadala lukuki kwenye mitandao ya kijamii
kuhusiana na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Wapo wanaharakati na
wanasiasa kadha wa kadha wamekuwa wakifanya jitihada za kutaka kutaja
majina ya walio nyuma ya biashara hii, lakini mwishoni hupatwa na
kigugumizi na kuishia hewani.
Marehemu Amina Chifupa (MB), aling'aka bungeni na kutangaza kwamba anayo
majina ya wanaojihusisha na biashara hii haramu na atayataja muda
wowote, lakini kwa bahati mbaya akatangulia mbele ya haki kabla ya
kutimiza azma yake hiyo.
Rais mstaafu wa awamu ya nne ya JMT, Mhe. Jakaya Kikwete alinukuliwa
akisema amepatiwa majina ya watu wazito wanaojihusisha na biashara hiyo,
lakini naye mpaka anaondoka madarakani, hakuchukua hatua zozote.
Yupo Blogger Mtanzania aishiye ughaibuni anayeitwa Mange Kimambi, naye
amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuhusu vigogo wanaojihusisha na
biashara ya madawa ya kulevya inayoangamiza vijana wengi na kuharibu
nguvukazi ya taifa, lakini mpk sasa Jeshi la Polisi na vyombo vya
usalama nchini vinaonekana kusua sua kulivalia njuga suala hili.
Leo, gazeti la Jamhuri limeandika orodha ya majina ya wanaohusishwa na
biashara hii ya madawa ya kulevya ambayo yamekabidhiwa kwa waziri wa
mambo ya ndani, Mhe. Charles Kitwanga ambaye ameyafikisha kwa Mheshimiwa
John Pombe Magufuli (kwa mujibu wa gazeti hilo).
Je, hii inatoa ishara njema ya 'kutumbuliwa jipu' hili la muda mrefu?
==================
Gazeti la JAMHURI leo limetangaza orodha ya wauza unga iliyokabidhiwa kwa Rais Magufuli
By MeinKempf
0 comments:
Post a Comment