Friday, December 4, 2015

Staa anayefanya vema katika soko la mziki wa bongo fleva,Kala Jeremih amefunguka juu ya kasi ya utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano Dr Magufuli kwa kusema kuwa inatia matumaini kwa wananchi.

Kala ambaye wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu,alikuwa moja kati ya wasanii waliokuwa wanamuunga ,mkono Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa,amesema yeye kama mwananchi anafurahishwa na jinsi Dr Magufuli anavyofanya kazi yake ya kuwatumikia wananchi.

Mkali huyo aliyewahi kuvuma na trak yake ya 'Dear God'amesema anaamini kasi ya Dr Magufuli itaendelea pia hata wakati wa kuwateua mawaziri na manaibu mawaziri ambao watakuwa na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi

0 comments:

Post a Comment