Msanii huyo anatarajia kushuka jukwaani na wimbo mpya ambao anatamba
nao kwa sasa alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi
Olomide, uitwao Acha Kabisa.
Mkali huyo mwenye kibao cha ‘Nashindwa’ anatarajia kufunga mwaka kwa
kukata kiu kwa mashabiki wake kwa kuimba na kucheza ngoma zake zote kali
kama vile Nani Kama Mama, Nakuhitaji, Msaliti, Nashindwa, Amerudi na
nyingine kibao.
Mashabiki pia wategemee kupata sebene la aina yake kutoka kwa Malaika
huku kukiwa na wakali kama Adaya, Petit Mauzo, Pilu, Mico Bella, Chesco
Vuvuzela, Yanick Soslo, Babu Bomba, Kadogoo Machine na wengine wengine
wengi.
Baada ya kufunga mwaka, katika Sikukuu ya Mwaka Mpya (Januari 1),
bendi kongwe ya muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’
ikiongozwa na Ali Chocky itakuwa na kazi moja ya kulishambulia jukwaa
kwa kutoa sebene la kisasa kwenye ukumbi huo.
0 comments:
Post a Comment