ALIYEKUWA Mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama kupitia CCM,kabla ya kulikosa jimbo hilo mara baada ya kuhamia CHADEMA,James Lembeli amesema kuwa anashindwa kuelewa ni kwa nini Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni anashindwa kufanya kazi zake ipasavyo.
Lembeli ambaye alijiunga CHADEMA kwa mbwembwe nyingi pamoja na aliyekuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Kagera,Ester Bulaya ,amesema kuwa mambo anayoyafanya Mkuu wa wilaya huyo machachari ni sawa na kutekeleza maagizo ya wakubwa wake
George Rugimbwana alikuwa mtu makini. Ikawaje akahamishwa Ukuu wa Wilaya Kinondoni? Ni wazi Makonda zero na yupo kwa maslahi ya aliyemteua.
— James Lembeli (@JLembeli) December 15, 2015

0 comments:
Post a Comment