Zaidi ya magogo ya asili 5000 pamoja na makontena 20 yaliyojaa magogo yamekamatwa na wakala wa misitu nchini katika mpaka wa Tanzania na Zambia mjini Tunduma, yakisafirishwa kinyume cha sheria huku yakiwa hayajulikani yanakotokea.
Magogo hayo yamekamatwa yakiwa kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia
mjini Tunduma kufuatia doria ambayo imefanywa na maofisa wa wakala wa
misitu nchini.
Mkurugenzi huyo wa wakala wa misitu nchini, Mohamed Kilongo amesema
mbali na magogo hayo pia wamezuia usafirishaji wa makontena 20 ambayo
yameingizwa nchini kutokea Zambia yakiwa yamebeba magogo, hatua
inayotokana na usafirishaji huo kukiuka makubaliano baina ya nchi hizo
mbili ya kutoruhusu usafirishaji wa magogo ya aina hiyo.
Hata hivyo meneja wa idara ya maliasili wa Zambia, Adotey Addo
amesema nchi yake imetoa kibali cha kuruhusu usafirishaji wa makontena
20 ya magogo, na kwamba mbali na makontena hayo, magogo mengine ambayo
yamekatwa ni haramu.
Baadhi ya mawakala wa kampuni za usafirishaji, Clearing and
Forwarding ambao wameshughulikia usafirishaji wa magogo hayo wamesema
sio jukumu lao kujua kama mzigo wanausafirisha ni halali au haramu kwa
kuwa hilo ni jukumu la idara ya forodha.
0 comments:
Post a Comment