Posted by Williammalecela.com on Friday, December 04, 2015
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo
waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kuhakikisha wanafanya kazi kubwa
kushindana na kazi ya rais John Magufuli.
Sugu alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha kumchagua diwani atakayewania nafasi ya Umeya kwa tiketi ya chama hicho.
Aliwataka madiwani hao kuchapa kazi na
kuwafanya wananchi kujivunia kasi ya maendeleo inayoletwa na Mbunge na
Meya wa jiji hilo ili wasitamani jimbo hilo lingeongozwa na wapinzani
wao wa CCM.
“Hata
CCM wenyewe wamebadilika, Magufuli anakwenda jalamba. Hakutakuwa na
vitu kama ambavyo mnaviwaza, tunaenda kufanya kazi za wananchi ili
wananchi wasitamani kwamba afadhali na hapa pangekuwa CCM. Waseme hata
kama Magufuli anaenda spidi na sisi Mbeya yetu Meya na Mbunge wanakwenda
spidi.”
0 comments:
Post a Comment