Serikali
imesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku 14 ili kuwapa muda wa
kutosha watu waliovamia na kuishi katika bonde la Mto Msimbazi Mkwajuni
kuondoka, ambapo imesisitiza kuwa baada ya siku hizo kuisha zoezi hilo
litaanza tena na hivyo wahakikishe wanaondoka wenyewe.
Akitoa tamko hilo waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh
William Lukuvi amesema waliojenga katika eneo hilo wapo hapo kinyume
na sheria kwa sabubu ni mahali hatarishi.
Akaongeza kuwa kuanzia mwakani wizara yake itagawa kwa viongozi wa
serikali za mitaa ramani za mipango miji ili waweze kuzisimamia kwa
ukaribu ili kuepusha uwezekano wa kutokea ama kufanya ujezi holela.
Aidha baadhi ya wananchi wamepongeza zoezi za bomoabomoa na kusema
kuwa imekuwa na hatua ngumu lakini muhimu kwani eneo hilo limekuwa
likisababisha vifo vya watu kila mafuriko yanapotokea hivyo watu
kuondolewa hapo wamenusurishwa kwa mengi.
Katika hatua nyingine waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Mh
Jenister Mhagama ameziagiza kamati za maafa katika ngazi za mikoa,
wilaya na vijiji kuorodhesha na kuwapa barua za kuwataka watu wote
wanaoishi maeneo hatarishi kuhama mara moja katika maeneo hayo na
utekelezaji wa agizo hilo uwasilishwe ofisi ya waziri mkuu haraka
iwezekanavyo.
0 comments:
Post a Comment