Waziri
wa mambo Nje Afrika Mashariki kikanda na kimataifa balozi Dk Agustino
Maiga amewaagiza wakurugenzi wa mashirikia yaliyo chini ya wizara hiyo
kuacha tabia ya kubuni miradi ya muda mfupi isiyo na tija kwa ajili ya
kuwafurahisha viongozi au waonekane kuwa wanafanyakazi na badala yake
wajenge miradi ya kudumu yenye maslahi kwa taifa na kizazi kijacho hata
kama utekelezaji wake utachukua muda mrefu.
Balozi Agustino Maiga ametoa kauli hiyo jijini Arusha katika ziara
ya kukagua miradi inayo tekelezwa na wizara ya mambo ya nje ambaye
ilianzia katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC na ujenzi wa
kituo cha kumbukumbu ya iliyokuwa mahakama ya kimbari ya Rwanda
kinachojegwa jijini Arusha na kutoa agizo ilo kwa wakurugenzi wa
mashihirika yaliyo chini ya wizara hiyo.
Mkurungenzi mtendaji wa kituo cha kimataifa cha AICC Elishiria
Kaaya amesema AICC imewapokea maagizo ya waziri na tayari ilishaanza
kutekeleza miradi imara na sasa kwa kushirikiana na wizara ya nishati na
madini wanajenga kituo kikubwa cha madini kitakacho hifadhi na
kuchakata madini ya vito bila kupeleka nchi za nje.
0 comments:
Post a Comment