Staa wa filamu Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’ hivi karibuni
alianika ‘mazagazaga’ yake aliyoyapamba kwenye kiuno chake alipokuwa
kwenye kibao kata cha ndugu yake kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Future
Resort, uliopo Mbezi Beach jijini Dar.
Davina ambaye alionekana mwenye furaha siku hiyo alivalia dera lake
ambalo kwa nyuma alilipasua na kuacha sehemu kubwa ya mgongo wake wazi
akiwa amejichora ‘tatuu’ huku cheni ya dhahabu ikiwa inaonekana.
“Duuh umemuona Davina hapo mgongoni kajichora vizuri na akigeuka kwa
mbele huwezi kujua kabisa kama nyuma yupo wazi lakini kwa upande wangu
mimi naona kapendeza sana,” alisikika mtu mmoja ambaye alihudhuria
katika sherehe hiyo.

0 comments:
Post a Comment