Kwa mara nyingine tena, mrembo wa Tanzania ameshindwa kunga’ara
katika mashindano ya mrembo wa Dunia. Katika fainali zilizofanyika jana
mrembo wa Tanzania, Lilian Kamazima, hakuambulia chochote.
Msindi wa Miss World 2015 ni binti mwenye miaka 23 toka Hispania
,Mireia Lalaguna Royo. Nafasi ya pili iliwenda kwa Mrusi , Sofia
Nikitchuk wakati nafasi ya tatu ilikwenda Indonesia ambayo iliwakilishwa
na mrembo Maria Harfanti.
Siku mbili zilizopita zilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii
kwamba Lilian Kamazima amefika kumi bora, lakini taarifa hizo si za
kweli. kumi bora katika michuano hii ilihusisha warembo toka mataifa ya
Urusi,
Ufilipino, Guyana, Lebanon, Hispania, Afrika ya Kusini,Ufaransa,
Australia , Jamaica na Indonesia.
Tangu mrembo Nancy Sumari aweke rekodi ya kuwa Miss World Africa, hakuna mrembo aliewahi kuifikia rekodi hiyo.


0 comments:
Post a Comment