Mtangazaji na msanii wa kundi la muziki wa dansi la Mapacha Watatu
ameeleza kuwa katika maisha yake ya kimuziki aliwahi kutunzwa kiasi cha
dola 1000 za kimarekani na kuongeza kuwa katika utunzwaji wa wasanii
kunachangamoto mbalimbali ambazo usipokuwa makini unaweza kujikuta
unamsaliti mkeo au mpenzi wako.
Akizungumzia changamoto hizo Jose Mara amesema kuwa unaweza ukatunzwa
kiasi Fulani cha pesa na kukuta pesa hizo zimeandikwa namba za simu za
aliyekutunza na kueleza kuwa upande wake Jose Mara amesema yeye hawezi
kushawishika kumsaliti mke wake kwani anamuheshimu na haitaji kuugua
maradhi yanayosababishwa na ngono nzembe.
Vilevile Jose Mara amevitaka vyombo vya habari kuunga mkono mziki wa
dansi kama wanavyofanya kwenye aina nyingine ya muziki kwani kutouunga
mkono ni kuua mziki huo

0 comments:
Post a Comment