Hospitali
za Apollo zimefanikiwa kwa mara ya kwanza barani Asia kufanya
upandikizaji wa moyo na ini; hivyo kujiunga na timu ya hospitali chache
duniani zilizowahi kufanya upasuaji huo wa aina yake.
Desemba
2015; Hospitali za Apollo ambazo ni kinara barani Asia kwa ubora wa
huduma za afya, kwa mara nyingine zimeonyesha ubora wake wa uongozaji
kupitia kituo cha upandikizaji duniani kwa kufanikisha upasuaji wa
upandikizaji kwa mpigo wa ogani za moyo na ini kwa kijana mwenye umri
wa miaka 30 anayetokea Tiruchengode, Tamilnadu nchini India. Tukio hilo linalotambulika kitaalam kama en-Bloc CHLTni
mfumo mgumu wa upasuaji na haujawahi fanyika popote barani Asia. Kama
ilivyoitwa na chuo cha Stanford kuwa ni “upasuaji wa kiufundi na
kitaalam sana, ambao ni vyema uachwe kwenye mikono ya madaktari bingwa
wenye ujuzi”, ni hizo hatua za CHLT pekee zimeweza kufanyika ulimwenguni
pekee.
Stori
hii ya Ndg. Ponnar, kijana mtulivu kutokea Tiruchengode, mji mdogo
kutokea wilaya ya Namakkal Tamilnadunchini India. Ponnar alikuwa ni
mwanafunzi bora aliyemaliza stashahada yake kwenye fani ya uhandisi na
alikuwa na medali ya dhahabu. Katika umri wa miaka 22, kama kijana
mwenye malengo makubwa na matumaini ya kufikia ndoto zake, Ponnar
alianza kuhisi kujaa maji tumboni mwake, upungufu wa pumzi na kujikuta
rangi ya ngozi yake kuanza kuwa manjano.
Hii
ilitambulika kama kufeli kwa ini, iliyopelekea kufanyiwa kwa
upandikizaji wa ini, ambao familia yake ilikuwa tayari kwa kijana huyo
kufanyiwa hilo zoezi la upandikizwaji. Wakati alipofika kwa ajili ya
kufanyiwa upasuaji huo wa kupandikizwa ini, iligundulika kuwa Ponnar
anatatizo katika mfumo wa upumuaji unaoitwa kitaalam Ebsteins anomaly au kufeli kwa upande wa kulia wa moyo katika kufanya kazi kwa usahihi ambao ndio awali umeletea udhoofu katika ini.
Bahati
mbaya kujumuika kwa matatizo mawili kwa mpigo kulimfanya Ndg Ponnar
kutokuwa na njia mbadala yoyote mbali na kujumlisha upandikizaji wa ini
na moyo. Hii ni hatua ya upasuaji inayohusisha njia kuu mbili kwanza
ya kupitia kooni na kifuani (kwa ajili ya moyo) na kupitia tumboni (kwa
ajili ya ini) hivyo kufanya zoezi kuwa hatari sana.
Ponnar-
kwa utulivu na ukakamavu alijiandaa kupigania uhai wake mpaka mwisho.
Familia yake hasa dada yake ambaye alikuwa tumaini na nguzo kwake,
maamuzi ya kwamba watafanya lolote liwezekanalo kuhakikisha wanamwokoa
kijana wao, walimpelekea hospitali za Apollo, Chennai, India.
“kwa
tatizo la kuwa na moyo usiofanya kazi ipasavyo, kulikuwa na presha
kubwa upande wa nyuma wa ini iliyosababisha kuharikika kwa seli za ini
iliyopelekea udhoofu huo wa ini. Kwa kuongezea, timu ya upandikizaji wa
ogani walijadili uwezekano mkubwa wa uvujaji mwingi wa damu hasa kwa
kuwa ni upasuaji wa sehemu mbili kwa mpigo na pia uwezekano mkubwa wa
sumu kujikusanya kwenye ini, kuathiri moyo hasa kama ogani hizo mbili
zitapandikizwa tofauti tofauti” alisema ”Dk. Paul Ramesh, mshauri
mwandamizi wa upasuaji katika mfumo wa upumuaji kutoka hospitali za
Apollo, Chennai.
Upasuaji na upandikizaji wa moyo na ini unaweza fanyika kwa njia kuu tatu;
1. Kwanza
upandikizaji wa moyo- ufuatiwe na upandikizwaji wa ini pale mgonjwa
atapokuwa amepata nafuu kutokana na upasuaji wa kwanza.
2. Kwanza upandikizwaji wa moyo- ufuatiwe na upandikizwaji wa ini kama njia mbili tofauti ila kwa mpigo katika operesheni moja.
3. Upandikizwaji wa moyo na ini kwa pamoja, inafanyika kwa ogani zote kuchukuliwa kama moja na kupachikwa kwa pamoja kwa mpigo.
Ni
wale mabigwa tu kwenye ile timu ya upandikizwaji wa ogani kufanya kazi
pamoja kama timu moja na kuleta matumaini ya kufanikisha en-bloc CHLT mfumo adimu sana kufanyika duniani.
”kwa
zaidi ya miongo ya ujuzi katika upandikizwaji wa ogani, imetuwezesha
kupata maarifa na utaalamu unaohitajika kufanya operesheni ngumu kama
hizi. Mafanikio yetu katika upandikizwaji wa moyo na ini yaliyopatikana
yametupatia msingi na uimara katika uendeshaji bora wa en-bloc CHLT kwa
bara la Asia. Najivunia sana kwa ajili ya Ponnar na familia yake
walioweza kuimanini timu kutoka hospitali yetu ya Apollo, imetupa sana
motisha sisi kuendelea mbele na mfumo huu bila mipaka ili kufika juu
kabisa. Aliongeza Dk. Ramesh.
Ponnar
alisubiri kutokea April hadi 0ktoba 2015 ili mtoaji damu anayemfaa
alipopatikana. Alifanyiwa upasuaji wa upandikizwaji huo wa moyo na ini
tarehe 14 oktoba 2015 na aliruhusiwa kwenda nyumbani ndani ya wiki baada
ya upasuaji huo. Leo hii, Ponnar ni mzima wa afya njiani kuelekea
kupona kabisa na kurudia maisha yake ya awali- ni mwenye furaha sababu
ngozi yake sio ya njano tena, na sasa anaweza kuendelea kufurahia raha
za maisha kama kutembea kwa miguu yake mwenyewe. Kwa maumivu yaliyokuwa
nyuma kwa miaka 8, sasa Ponnar yupo huru kuendeleza matumaini yake na
ndoto zake.
Ngazi
hii ya kimatibabu, ya upandikizwaji wa moyo na ini kwa mpigo (mara ya
kwanza barani Asia) ni hazina kubwa kwa Ndg Ponnar na dada
yake,walioweza kutosikiliza uzushi wa watu wote. Pia ni ushuhuda kuwa
timu ya madaktari wa upandikizwaji kutoka hospitali za Apollo Chennai
wamefanikiwa kufanya operesheni hii kwa mafanikio makubwa. Haya yote
yasingeweza kufanikiwa kama pia kusingekuwepo kwa ushirikiano mkubwa
kutoka serikali ya Tamilnadu na programu ya kujitolea ogani iliyopo
Tamilnadu ambayo imesifiwa ulimwenguni kwote kwa kazi kubwa walioifanya.
”mafaniko
haya makubwa ni agano kwa mabingwa wote wa upasuaji duniani, madaktari,
wataalam, manesi na wafanyakazi wote waliojitolea kuwahudumia wagonjwa
na kutoa huduma zilizopo katika viwango vya kimataifa. Upasuaji ni
matokeao ya mipango bora iliyofanywa kwa siku kadhaa kutoka kwa timu ya
wataalam upande wa moyo na ini na uonekanaji wa miundo mbinu bora na
wataalam waliokubuhu. Jitihada hizi shirikishi zinachukua timu zote za
upandikizaji ili kutathimini na kuweka mikakati kasha kuonyesha kuwa
fani hii ni ya kuheshimika”. Alisema Dk. Prathap C Reddy, mwenyekiti na
mwanzilishi wa Hospitali za Apollo

0 comments:
Post a Comment