Sunday, December 27, 2015

 
Mchungaji wa kanisa moja huko nchini Nigeria, amewatoa machozi ya furaha waumini wake katika siku ya Ibada Jumapili, baada ya kugawa kapu la chakula kwa kila muumini aliyehudhuria siku hiyo.

Mchungaji huyo aliwatunuku waumini wake, kilo kadhaa za mchele, viungo, mafuta ya kupikia, kuku mzima kwa ajili ya kitoweo na vikolombezo vingine vingi.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo, walionesha kufurahishwa na hatua hiyo huku wakikiri kuwa itaongeza hamasa ya kupenda ibada.

0 comments:

Post a Comment