KIBANO! Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limemnasa mkulima mmoja, Kiliani
Fussi (pichani) kwa tuhuma za kulima bangi kwa kificho kwenye shamba
lake maalum huku akijua ni kosa kisheria, twende na Risasi Jumamosi.
Zoezi hilo lilifanyika hivi karibuni ambapo mkulima huyo alishtukizwa na
askari akiwa kwenye shamba hilo lenye ukubwa wa nusu eka ambalo lipo
kwenye Mtaa wa Namanyigu katikati ya Manispaa ya Mji wa Songea.
Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela
na Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa, Revacus Malimi walilifikia
shamba hilo kwa tabu kwani njia ya kuelekea ilikuwa ina majani aina ya
upupu ambayo yana sifa ya kuwasha hali iliyowalazimu polisi hao
kuyafyeka kwanza majani hayo ili kuweza kupita kwa urahisi.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo kwa nyakati tofauti waliliambia
Risasi Jumamosi kwamba, Fussi amekuwa mkulima wa siku nyingi wa mmea
huo haramu lakini huwa analindwa na baadhi ya viongozi licha ya raia
wema kutoa taarifa.
Walisema kuwa, majirani wenzake ambao wanalima katika eneo moja mazao
ya chakula na biashara walijaribu kumuonya kuhusu ulimaji wa zao hilo,
lakini hakuwasikiliza.
Kama kawaida yake, Risasi Jumamosi lilimdaka Kamanda Msikhela ili
aweze kuzungumzia sakata hilo la ukomeshaji wa kilimo haramu cha bangi
nchini ambacho kimekuwa kikileta madhara makubwa kwa jamii ambapo
alisema:


0 comments:
Post a Comment