Saturday, December 12, 2015

Yatosha

Msanii anaefanya poa kitaifa na kimataifa Diamond Platnumz ameachia video ya ngoma yake ya Je Utanipenda nyimbo ambayo ameimba kwa hisia kubwa pia nyimbo ambayo ameifanya kwa mtayarishaji Tudd Thomas na  video kuandaliwa na mtayarishaji mahiri Godfather, video hiyo imefanyiwa jijini Dar es Salaam na Johanesburg nchini Afrika Kusini.IMG_20151212_071813
Watu wengi wamekuwa wakijiuiza kwanini msanii Diamond ameamua kuachia wimbo huo je utanipenda, kupitia ukurasa wake wa You tube  Diamond amesema kuwa huo ni wimbo unazungumzia maisha yake halisi, ni wimbo ambao Diamond anamuuliza mpenzi wake Zarina Hassan kuwa itakuwaje kama atapoteza kila kitu alichonanacho kwa sasa ikiwemo magari,nyumba umaarufu na vingine vyenye kufanana hivyo na kumuuliza JE ATAMPENDA?IMG_20151212_071758

1 comment:

  1. Nyimbo nzuri sana huwa hakosei Diamond ila hii ishu ya kuimba maexi wake angeachana nayo tu ila hongera sana.

    ReplyDelete