Tuesday, December 22, 2015

Mtela Mwampamba

Katika watu ambao kwa hakika walimwandama sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ni Saed Kubenea kupitia magazeti yake ya Mwanahalisi na MAWIO.
Pia Kubenea amekuwa akitumia mitandao yake ya kijamii ukiwemo mtandao wa Mwanahalisiforum kumsakama Kikwete na Serikali yake.
Moja ya hoja alizokuwa anatumia Kubenea ni kukithiri kwa ufisadi na mafisadi. Kwamba,, Kikwete amewalea sana mafisadi na CCM ni chama cha mafisadi. Kubenea hakuacha kumuandama Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi wa Richmond, Edward Lowasa.
Sikufikiria kuwa itafikia wakati Kubenea atakuwa ni rafiki wa ufisadi na mafisadi. Sikutegemea kuwa kuna siku magazeti ya
Mwanahalisi na MAWIO yatatumika kuwatakasa mafisadi. Baada ya kumtakasa Lowasa na kashfa za ufisadi wa Richmond, sasa Kubenea na Magazeti yake ya Mawio na Mwanahalisi yanatumika kumsafisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mussa Natty ambaye kwa hakika hakustahili hata kuwa kiongozi wa umma. Kubenea sasa haoni jinsi barabara za Kinondoni zilivyojengwa kwa kiwango cha chini na kwa gharama kubwa kiasi ambacho barabara hizo zinabomoka hata kwa kupigwa na matone ya mvua.
Kubenea sasa haoni jinsi maeneo ya wazi yalivyouzwa kwa njia ya kifisadi huku wananchi wengi wakilalamika utendaji mbovu wa Ofisi ya Ardhi huku Mussa Natty akishindwa kuchukua hatua.
Yaani sikutegemea kabisa. Kweli wana Ubungo wamekula hasara. Kuwa na mbunge ambaye anakumbatia uovu na waovu hakika ni jambo la kujilaumu kwa maamuzi waliyofanya




0 comments:

Post a Comment