Kocha
wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm
|
Kocha
wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm mpango wake mpya alionao sasa ni
kujaribu kuwapa nafasi na kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa
hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika michuano
ya Ligi Kuu Bara.....,
Lakini
mkakati huo utaanza kutumika kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi
itakayoanza rasmi Januari 2, mwakani huko visiwani ikiwemo kuendelea
kuangalia zaidi kasi za wachezaji wapya waliosajiliwa kikosini humo hivi
karibuni.
Pluijm
amesema kuwa nia yake ni kushindana lakini pia itakuwa ni fursa nzuri
kuwapa nafasi vijana wengine wakiwemo wale waliopandishwa hivi karibuni
wakitokea kikosi cha timu ya vijana maarufu kama Yanga B.
“Tutakwenda
kupambana kama ilivyo kawaida huwezi kusema kwamba utachukua ubingwa
kama hutaweka nia ya kufanya vizuri kwenye michezo ya awali, hivyo
tutatumia ushindi wa kila mchezo ili kufikia hapo tunapopataka."
“Lakini
pia itakuwa fursa nzuri ya kuangalia vijana wengine ambao wamekuwa
hawapati nafasi ya kutosha kwenye ligi na michuano mingine nao kutumika
na kuonyesha zaidi, taratibu kutakuwa na mchanganyiko lakini nia ni watu
kupata nafasi pia.
“Kwenye
kundi letu tupo na Azam, Mtibwa pia, tunatoka ligi moja lakini kwenye
mashindano haitakiwi kuogopa kitu, tutakutana nao na nia yetu ni
kushinda,” alisema Pluijm aliyeiongoza Yanga SC kutwaa ubingwa wao wa 25
msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment