MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa
halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko
katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchi.
Sadiki
amesema utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya
Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa
ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu
.“Siwezi
kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo
wanayofanyiashughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na
kutupa ovyo,” amesema.
Amesema
viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi,
wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao
wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.
Aidha,
ameiiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaondoa wapigadebe katika
vituo vya daladala kwani wamekuwa kero kwa abiria.

0 comments:
Post a Comment