Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Akutana na wadau wa Elimu wilaya ya same wakiwemo watendaji Elimu mkoa, wilaya, watendaji tarafa na kata, waratibu Elimu kata , wakuu wa sekondari wote na wadau wengine wengi.
Amewaeleza wadau wa Elimu kuwa Matokeo ya darasa la saba yaliyotoka mkoa wa Kilimanjaro umefanya vizuri kwa kushika nafasi ya 4 Kitaifa
Ameagiza yafuatayo
1. Watoto wote waliofaulu wahakikishe wanakwenda Shule, na utekelezaji wa elimu bure utekelezwe kwa mujibu wa waraka wa serikali
2. Watoto wote watoro wasakwe popote walipo na wapekekwe Shule na wazazi watoe ushirikiano
3. Fedha zote zitakazotolewa kwa ajili ya shughuli za Shule zitunzwe na waepuke kubadilisha matumizi
4. Ameagiza tatizo la madawati katika mkoa wake mwisho April kila halmashauri ijitoshekeze kwa madawati na afisa misitu amekubali kutoa Kibali cha kukata miti kwa ajili ya madawati.
5. Amehaidi kuanza operesheni ya kufyeka mashamba ya mirungi yote wilaya ya Same ambayo kiasi Fulani wadau wameeleza kuwa baadhi ya wanafunzi wamefeli kwa kujihusisha na mirungi.


0 comments:
Post a Comment