Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) litamfikisha kwenye Kamati
ya Maadlili mapema Mwakani baada ya sikukuu ya mwaka Mpya 2016, Mkuu wa
Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutokana na kauli zake za
kibaguzi dhidi ya Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.
Muro alimshambulia kwa maneno ya kibaguzi Manara wakati akizungumza
na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika jana makao makuu ya
klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam.
Kauli ya Muro dhidi ya Manara ni kinyume na Katiba ya TFF, Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) ambao zinapiga vita vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote
katika mpira wa miguu.
Mapema mwaka huu, Muro alifikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF
kutokana na kumshambulia na kumdhalilisha kupitia vyombo vya habari
aliyekuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB),
Fatma Abdallah. Kamati ya Nidhamu ilimwadhibu kwa kumpiga faini ya sh.
milioni 5.
0 comments:
Post a Comment