
Muimbaji huyo ambaye pia ni mwandishi mzuri wa nyimbo, ameiambia Bongo5 kuwa video nyingi za wasanii zilizotoka zimemfanya aweke zake kapuni ili atoe mwakani.
“Mwaka huu hatuwezi tena kutoa video kutokana na population ya wasanii kutoa video. Watu wanaojua marketing ya muziki wanajipanga na kuangalia muda sahihi wa kuachia video. Nashukuru Mungu video zipo tayari na good news ninaweza kutoa video mbili moja ya kolabo yangu na Chameleone na nyingine itakuwa mpya na zote nimeshoot nje,” alisema Barnaba.
Pia muimbaji huyo amewashukuru mashabiki wa muziki wake kwa kupokea vizuri wimbo ‘Nakutunza.’
CHANZO;BONGO5
0 comments:
Post a Comment