Peter
Msechu ni miongoni mwa wasanii wachache ambao hawaoni shida kukiri kuwa
si wazuri kwenye upande wa uandishi wa nyimbo, licha ya kuwa na kipaji
na uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza vyombo vya muziki.
Baadhi ya wasanii (wa Bongo) huwa hawapendi kusema ukweli pale
wanapoandikiwa nyimbo na wasanii wengine, kwa kudhani watu wakijua
wameandikiwa inaweza kuwapunguzia thamani.
Msechu ambaye ameachia wimbo mpya wiki iliyopita, amesema kuwa baada
ya kugundua kuwa sio mzuri kwenye upande wa uandishi wa nyimbo, sasa
hivi nyimbo zote atakazorekodi atakuwa anawapa watu wengine kazi ya
kuandika na kumpa njia na sauti ya kuimbia (melody).
“Unajua nimekuja kugundua kuwa nilikua sijitambui, nilikua
nalazimisha kuandika nyimbo kitu ambacho nilikuja kugundua kuwa mimi sio
mzuri upande huo.” Alisema Msechu kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.
Msechu aliongeza kuwa wimbo wake ‘Nyota’ ambao wote aliandikiwa na
Amini ndio umetokea kuwa wimbo mkubwa na uliompa mafanikio kuliko
nyimbo zote alizowahi kufanya.
‘Nyota’ ndio wimbo ambao pia ulimpa nafasi Msechu ya kutajwa kuwania
tuzo za Kimataifa za AFRIMA 2014 za Nigeria kwa mara ya kwanza.
Wimbo mpya alioutambulisha wiki iliyopita ‘Malava; umeandikwa na
Barnaba. Msechu amefungua milango kwa msanii au mwandishi yeyote
anayehitaji kumwandikia nyimbo yupo tayari kufanya naye kazi.
0 comments:
Post a Comment