Peter Msechu amekiri kuwa nyimbo zake za mwanzo hazikufanya vizuri kwasababu zilikuwa zikokiufundi sana, lakini ‘Nyota’ ndio ilikuja kumpa majibu kwamba mashabiki wa Tanzania wanataka nyimbo nyepesi zinazoweza kukaririka kirahisi.
Msechu ameyasema hayo alipozungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio wiki hii.
“Kimuziki bado jamii yetu haijaelewa muziki wa professional…raia wa kibongo wanataka akiwa anapiga deki mmama akisikia chorus aimbe huku anapiga deki, lakini sio aanze kuhangaika kuimba ma high pitch manini, watu wanafanya professional mimi nafanya show za live nina arrange miziki mikubwa tu lakini huo ni muziki ambao ukafanye mbele, kwa hapa kuna muziki wao wanaoutaka” alisema Msechu.
Msechu ameongeza kuwa anazo nyimbo nyingi alizorekodi kwa utaalamu mwingi na zilizo mgharimu kiasi kikubwa cha pesa, lakini amelazimika kuziweka zibaki kuwa za kusikiliza mwenyewe nyumbani.
“Mimi kabla sijatoa hii malava nimerekodi nyimbo karibia 17, ni nyimbo ambazo zote siwezi kuzitoa kwasababu nyingine nimezikunja, production kuna nyimbo moja nimetumia karibu milioni 3 kurekodi hiyo nyimbo, kwasababu nilipiga kila kitu kitu live, hadi kuna wapiga saxophone nimewatoa Uganda nikawaleta, lakini ile nyimbo itabakia ni nyimbo yangu tu mimi nikiitoa sitaeleweka kwasababu ni nyimbo ambayo iko mbali sana kibongo bongo wanataka muziki laini.” Alisema Peter Msechu.
0 comments:
Post a Comment