Kuna baadhi ya watu huenda hawafahamu kuwa mdundo wa ‘Nana’ wa Diamond Platnumz ni zao la producer Nahreel wa The Industry, na hii ni kutokana kwamba haina ule utambulisho wa kazi zake ‘Nahreel on the beat’ ambao husikika kwenye kazi zote alizotayarisha.
Nahreel amesema kuwa kiashirio cha producer kwenye wimbo huo kiliondolewa kwa sababu ambazo hakuona kama zina uzito.
“Sababu walizosema walisema tu stori ilivyoanza pale mbele ile slogan yangu ingeleta hitilafu lakini it doesn’t make sense, kwa hiyo ndo walitoa hiyo sababu lakini mimi niliona it doesn’t make sense hata kama hiyo slogan ingekuwepo isingeharibu chochote” Nahreel alisema kupitia Planet Bongo ya EA Radio.
Kutokana na kitendo hicho Nahreel amewashauri watayarishaji wengine kuwasainisha wasanii mikataba itakayowabana wafate makubaliano ya kazi ikiwemo kutoondoa utambulisho wa mtayarishaji kwenye beat.
“Kwanza sisi maproducer wenyewe tuwe strong kwenye hili suala, tukazie msanii anapokuja studio hizo slogan lazima kuweka hata na mkataba fulani kwamba hii slogan lazima iwepo, ukitoa hii kazi is no longer yours, kuwe na kitu fulani ambacho kinaweza kumbana msanii, kwa hiyo tuanze kuwabana wasanii hapa studio na kukubaliana kabisa”, alisema Nahreel.
dj mustard aseme hivyo na wewe useme hivyo tafuta slogan tako uache kuiga ndio mana dogo aliifuta sababu nyimbo zake zinasikuluzwa na watu wengi sasahv!buni slogan yako acha kuiga
ReplyDelete