Majira ya saa 10 na dakika 10
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo alifika katika mitambo ya
kuzalisha umeme wa gesi iliyoko Tegeta jijini Dar es Salaam
inachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na kukuta wafanyakazi
pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme wakiendelea na kazi katika
mitambo hiyo.
Waziri Muhongo amekagua mitambo
hiyo leo na kubaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa gharama ya
shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni kiwango
kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.
Pia Muhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na nishati hiyo hapa nchini.




0 comments:
Post a Comment