Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. William Ole Nasha Ikulu jana.
Mahmoud Ahmad Arusha
Nasha ambaye uteuzi huo ulivyotangazwa rasmi kwenye vyombo vya habari ulimkuta katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro hali iliyowashangaza wengi kwani hawakuwa wametarajia kuwa uteuzi huo ungetokea.
Akizungumza katika baraza la Madiwani Nasha alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kuwa hatawaangusha Watanzania kuwa hana rekodi ya kukosa maadili.
“Umakini mkubwa umetumika kuteua baraza la Mawaziri mpaka leo hii Mheshimiwa Raisi hajamaliza kuteua baraza , ni heshima kubwa sana kwangu namshukuru Magufuli kwa dhamana hii kubwa “ Alisema Nasha
Nasha amesema kuwa atashirikiana na wataalamu kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo katika taifa la Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda ambaye alikuwepo wilayani hapo katika ziara yake ya kikazi ya siku 3 amempongeza Mbunge huyo wa Ngorongoro ambaye kwa sasa ni Mbunge Mteule wa Ngorongoro.
Ntibenda amesema kuwa anaamini kupitia uteuzi huo utasaidia kuinua sekta ya ufugaji kutoka kwenye ufugaji wa kienyeji hadi kwenye ufugaji wa kisasa utakaoleta tija na kuinua uchumi wa wafugaji na taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo leo jimbo la Arusha mjini linafanya uchaguzi mdogo wa ubunge baada ya kuahirishwa kufuatia kufariki dunia kwa mgombea wa ACT Wazalendo Estomii Malah huku uchaguzi huo ukionekana kudorora kwa wakazi wa jimbo hilo kusuasua tofauti na hamasa iliyokuwapo kwenye uchaguzi mkuu hapo october 25.
Baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wameonekana wakiendelea na shughuli nyingine kana kwamba hakuna uchaguzi hali inayoleta sintofahamu hadi ifikapo mwisho kama kutakuwa na idadi ya wakazi waliojitokeza kwenye uchaguzi mkuu wa wabunge,madiwani na Uraisi.
0 comments:
Post a Comment