RAIS wa awamu ya tano Dk. John Magufuli, ametoa zawadi ya
vyakula, mbuzi na mafuta ya kupikia zenye thamani ya Sh mil 8,089,
000 kwa watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi,watu wenye ulemavu pamoja na wazee.
Akikabidhi msaada huo katika kituo cha kulelea watoto
wanaokinzana na sheria kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam, kwa niaba
ya Dk. Magufuli, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira Mushi, alisema
katika kusheherekea sikukuu za maulid,Chrismas na mwaka mpya Dk
Magufuli ameamua kutoa zawadi katika vituo nane katika mkoa wa Dar es
Salaam , viwili Zanzibar na Vituo Vitano toka mikoani kwa Tanzania
Bara.
Alitaja vituo hivyo kuwa ni Makao ya Taifa ya watoto yatima
Kurasini,mahabusi ya watoto Upanga kilichopo Ilala,Makao ya Wazee na
wasiojiweza Nunge Kigamboni,Chuo cha Ufundi kwa watu wenye ulemavu
Yombo, Kituo cha Mother Theresa Mburahati Kinondoni,Kijiji cha Furaha
Mbweni kilichopo Kinondoni, Dar al arqum Tandika (Temeke) na kituo cha
watoto Msimbazi, Kwa Zanzibar kituo cha Maboani Chakechake Pemba na
Cha wezero Unguja.
Alisema kwa mikoa ya Tanzania Bara vituo vilivyopatiwa
msaada ni Makao ya watoto Kemondo(Bukoba), Kituo cha Village of
Hope(Dodoma),Shule ya maadirisho Irambo(Mbeya), Makazi ya wazee
wasiojiweza Bukumbi,Misungwi(Mwanza) na Makazi ya wazee wasiojiweza
Sukamahela, Manyoni, (Singida).
“Lengo la Dk. Magufuli kutoa zawadi hiyo ni kuwawezesha
makundi hayo ya weze kusheherekea sikukuu kama ilivyo kwa watu
wengine.”alisema Mushi.
Meneja wa mahabusu ya watoto Upanga, Ramadhani Yahaya alisema
wanamshukuru rais Dk. Magufuli kwa ukarimu wake hasa kuwakumbuka watoto
wa ukinzani wa sheria na kudai kuwa mara nyingi wadau wamekuwa
hawawakumbuki.
“Tunawaomba wadau wengine wawe na moyo wa kuwasaidia watoto
hawa, pia tuna matatizo ya ufinyu wa bajeti katika serikali kunahuduma
muhimu ambazo tunazikosa tunaomba wadau mbalimbali wajaribu kusaidia
kutujengea uzio kwakuwa serikali itachukua muda kutatua tatizo
hilo”.alisema Mushi.

0 comments:
Post a Comment