Wanamuziki Justin Bieber na Taylor
Swift ndio waliotamba zaidi kwa mazungumzo katika mtandao wa kijamii wa
Twitter mwaka 2015, wakuu wa Twitter wamesema.
Kwa miezi sita ya kwanza, Taylor Swift ndiye aliyetawala kabla ya Justin Bieber “kuchukua usukani”.
Lakini mazungumzo katika mtandao wa Twitter haujakuwa kuhusu wasanii pekee na muziki.
"Mazungumzo
ya kisiasa na watu wakieleza hisia zao pia vimeongezeka,” mkuu wa
Twitter Ulaya Bruce Daisley aliambia kipindi cha Newsbeat.
"Ndiye msanii wa tatu kwa kuwa na wafuasi wengi Twitter. Nusu ya pili ya mwaka, Justin Bieber alitawala,” anasema Daisley.
"Bieber ndiye wa pili kwa kuwa na wafuasi wengi. Alikuwa na wafuasi 50 milioni na amewatumia vyema na kwa werevu.”

0 comments:
Post a Comment