Serikali
imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watendaji walioshindwa
kudhibiti ujenzi holela kwenye maeneo ya wazi,taasisi za umma na
kuwataka wananchi kuhamisha mali za thamani pamoja na kubomoa majengo
yao kwa hiyari kabla hawajavunjiwa kwa kuwa operesheni ya bomoabomoa
inaendelea hapa nchini bila kujali uwezo wa mtu.
Tahadhari hiyo imetolewa na naibu waziri,wizara ya ardhi,nyumba na
maendeleo ya makazi Mh.Angeline Mabulla wakati akizungumza maeneo
ya Buswelu wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza amesema kuwa watendaji wa
serikali waliohusika kusababisha migogoro ya ardhi ofisi yake
haitawavumilia kwa kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kuwataka
kushiriki kikamilifu katika zoezi linaloendelea la bomoabomoa kwenye
maeneo yao.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mwanza bw.magessa mulongo
akizungumza katika kikao cha watendaji kilichohusisha madiwani wa
halmashauri ya manispaa ya Ilemela amesema kuwa ofisi yake imebaini
baadhi ya watendaji idara ya ardhi wanahusika kusababisha migogoro na
kuwata wajihuzuru kabla ya kufukuzwa na kushitakiwa.
0 comments:
Post a Comment