Serikali imeitangaza rasmi siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya usafi na kwamba hatua za kisheria na kinidhamu zitachukuliwa kwa watendaji wowote watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo.
Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na naibu waziri wa ofisi
ya makamo wa rais, muungano na mazingira Bw Luoga Mpina ambapo amesema
agizo hilo linaanza mara moja huku akisisitiza kuwa lengo kubwa ni
kupambana na magonjwa yanaweza kusababishwa na uchafu.
Kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi waziri Mpina amesema
Tanzania hupoteza zaidi ya heka laki nne za misitu kila mwaka huku joto
la dunia likiongeza kwa nyuzi joto 0.85, ambapo pia kina cha bahari
kikiongeka hadi kufikia 19 cm, pia akatumia fursa hiyo kutoa agizo kwa
halimashauri zote nchini.
Kwa mujibu wa taarifa za wizara hiyo ya makamo wa rais muungano na
mazingira, Tanzania inazaidi ya hekta milioni 48.1 za misitu ambayo
hutumika kumeza hewa ya kabon tirion 9.03 ambapo juhudi za upandaji miti
zikitajwa kusaidia kuondoa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

0 comments:
Post a Comment