Tuesday, December 22, 2015

MBOWE UNAJUA USEMACHO...??? AMA UMETOKWA NA KUMBU KUMBU?


Ukitaka kujua kuwa Wapinzani wamekosa HOJA ya msingi ya kusimamia, usipate taabu sana! Msikilize mtu mmoja aitwaye Freeman Aikael Mbowe. Huyu ndiye Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani nchini, kwa vyovyote vile kauli zake zinatafsiriwa kuwa kauli za chama.

Wiki moja iliyopita nilipata kusikia kauli ya Freeman kuhusu utendaji kazi wa Rais Magufuli,sikufikiri kama nilimskia Mbowe sawasawa! Mbowe kupitia kauli yake analieleza Taifa kuwa Rais Magufuli anatekeleza Ilani ya Chama Chake. Mbowe anasisitiza kuwa, kudhibiti matumizi ya serikali na kupinga uhujumu wa Uchumi wetu ni kutekeleza Ilani yao iliyowekwa katika Website mwishoni mwa mwezi August mwaka huu.(Haieleweki vizuri kama ipo ama la!)

Baada ya kumsikiliza Mbowe,kama ilivyo kawaida yangu nilimpuuza kwani nilikwisha kuzoea kukosa maana katika maneno yake. Niliamini kuwa Mbowe hakujua anasema nini kwa sababu atakuwa anasumbuliwa na hang-over ya uchaguzi. Nilifikia hatua hiyo kwa kuwa sikumbuki ni wapi na lini Mbowe alianza kumtambua DR.John Magufuli kama Rais wa Nchi hii! Kama si sheria ya Mitandao ningesema Mbowe ni Mjinga kwa sababu anajitukanisha mwenyewe.

Jibu la Mjinga ni UKIMYA. CCM wakakaa kimya wakiamini kuwa ukimya wao utalinda heshima ya Mbowe.
Ikawa kama karogwa tena, Mbowe akaona anapata kick kwa kutangaza utekelezaji wa Ilani unaofanywa na Rais John Pombe Magufuli. Jana Mbowe kajitwika kazi ya usemaji wa Chama chake na Chama cha Mapinduzi kwa pamoja. Gazeti likaandika "MBOWE;JPM ANACHEZA NGOMA YA CHADEMA" hapa ndipo nikaamini kuwa Mbowe hafikiri vizuri kama ilivyo kwa Julius Mtatiro.


Kwa kawaida ukieleza utekelezaji wa Ilani yako inayotekelezwa na Rais anayetokana na chama kingine bila kujijua utakuwa unaeleza uvivu wako wa kufikiri. Mbowe anataka kuiaminisha Dunia kuwa CCM walijiandaa kutekeleza uovu katika nchi hii na hivyo Chama chake ndicho chenye kujua Matatizo ya Watanzania pekee!
Unaweza kusema kuwa Mbowe hajui kusoma na kama anajua kusoma basi hatimizi wajibu wake kama Mwenyekiti wa Chama. Kwa nafasi yake,si rahisi kuamini kuwa Mbowe hajaisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020. Ikiwa Mbowe kaisoma Ilani ya CCM, ni dhahiri kuwa anatambua kinachotekelezwa na Rais kinatokana na mwongozo wa Ilani hiyo. Kwa kutambua hilo,anapowaaminisha Watanzania kuwa Rais anatekeleza Ilani ya Chama chake,ni kwamba Mbowe anaendeleza tabia ya kuwadharau Wananchi na kuwafanya wao hawawezi kufikiri na kutambua mambo.


Najua CCM hawawezi kumjibu Mbowe kwa kuwa wanamdharau na kumpuuza kama mimi, isipokuwa ni kweli kuwa jambo likisemwa na lisijibiwe hupelekea watu kuamini hata kama ni uongo! Mimi nataka Mbowe na Mtatiro waeleze ni lini walianza kumtambua Dr. John Pombe Magufuli kama Rais wa Nchi hii ili tuanze kujadili hoja zao kwa utambuzi kuwa tunajadili utendaji wa Rais.
 

Pia, Mbowe atuambie ni wapi ilipo hiyo Ilani yao (UKAWA) inayotekelezwa na Rais Magufuli. Maana ni kweli kuwa katika kipindi chote cha Kampeni Ukawa hawakuwahi kuwa na Ilani ya Uchaguzi.

Kwa kuwa Mbowe haijui Ilani ya Uchaguzi ya CCM,pia hamtambui Rais lakini anatambua utekelezaji wake,ni dhahiri kuwa Mbowe hajui asemacho.
 

Sisi Watanzania tunapaswa kujiuliza kama yanayotekelezwa na Rais Dr. John P. Mgufuli sio agenda katika maendeleo yetu. Ukawa wanalitakia nini Taifa hili na hata utekelezwaji wa mambo mazuri uzue hoja?
 

Ni wazi kuwa UKAWA wanatamani Rais apuuze agenda ya wa Watanzania ili wao wapate hoja ya kuzungumza majukwaani! Kwa Mbowe propaganda ni muhim zaidi kuliko maisha ya Watanzania. Anachukia tunapobana Matumizi,kutoza kodi na kusimamia shughuli za serikali kwa kuwa hawatakuwa na hoja.Kwa hali hii Mbowe ana akili chafu kuliko hata Shetani,anatamani kila siku tuwe matatizoni! Tunamshauli Mbowe kuwa wakati wa Siasa umekwishapita,sasa tuijenge Nchi yetu.

Mwisho, naomba kumkumbusha Mbowe kuwa ni yeye ndiye anaecheza ngoma ya JPM. Alichezeshwa ngoma hiyo kwa siku 65 za kampeni,akakubali kucheza,akashindwa!
Watanzania wamekwisha tambua utoto wake,wanamkubali Rais wao kwa kuwa anatekeleza Matakwa yao na hivyo Mbowe akae kimya asitupotoshe WATU.

0 comments:

Post a Comment