Kapteni wa bongo fleva Tunda Man ambaye kwasasa anayangaza wimbo wake mpya wa ‘Mama Kijacho’ amesema wakati anafanya show kwenye kampeni za Siasa, Baba mwenye nyumba alimfukuza sababu alikuwa chama tofauti.
Tunda anasema “Kipindi hicho tukifanya kampeni za Magufuli, Baba mwenye nyumba wangu alinirudishia kodi ya mwaka mmoja na miezi sita, sababu ilikuwa mimi kufanya kampeni hizo,alinionyesha picha nikiwa kwenye stage na t shirt ya Magufuli, nilijua utani, ila mzee alinikazia siku nzima, nikabidi niondoke tu na nikahamisha vitu“.
Tunda Man anaendelea kusema baada ya kuhama nyumba hio na uchaguzi kuisha “Namba ya huyo mzee nilibaki nayo na siku tano zilizopita kanipigia na kuniomba nirudi,mzee amekuwa mtu wa Magufuli, nikamwambia kuna maisha baada ya uchaguzi“
0 comments:
Post a Comment