Bongo Fleva super staa Tunda Man ambaye kwa sasa anatangaza wimbo wake mpya wa ‘Mama Kijacho’ amesema wimbo huu sio wa mapenzi tu ila ni kile kinachotokana na mapenzi ambacho ni ujauzito na kuwa na familia.
Akihojiwa kwenye #FridayNiteLive East Africa Tv kuhusu mahusiano yake na Matonya, Tunda Man anasema kwa sasa hawako vizuri tena toka ampigie simu kuhusu kufanya video na Matonya alimjibu kwa kumtukana matusi .
“Nilimpigia simu ilitupange kufanya video ya wimbo wetu ila jamaa alinitukana sana na mimi nikasikiliza tu alivyomaliza nikakata simu“.
0 comments:
Post a Comment